MCHAKATO wa Chama cha
Mapinduzi CCM kumpata mgombea uenyekiti wa kijiji cha Kihangaiko tarafa ya
Msata Wilayani Bagamoyo mwishoni mwa wiki umeiingia dosari baada ya wajumbe wa
mkutano huo kunusurika kuzichapa hadaharani wakati kila kindi likitaka mgombea
wake apite.
Ngumi zilibuka mkutanoni
hapo baada ya msimamizi wa uchaguzi huo kutoka Kata hiyo Adamu Kitegire
akiungwa mkono na wana-ccm kutoka tawi la Madesa kutangaza kuahilisha mkutano
huo na kuzichoma moto kura zilizokuwa zimepigwa kuwachagua wajumbe wa serikali
kwa madai kuwa wanachama waliopiga kura hizo hawakuwa halali.
“naahirisha mkutano huu wa
mchakato kupata wagombea hadi hapo itakapopangwa tena,sababu kubwa ni kuwa
kwanza wengi wenu hapa sio wanachama halali wa CCM hivyo hatuwezi kuendelea”alisikika
Kitegire.
Kufutia makauli hiyo nae
mwenyekiti wa ccm tawi la Kihangaiko Mohamedi Kisulu akiungwa mkono na
wanachama wake alikataa na kumtuhumu msimamizi wa uchaguzi huo kuwa anakusudia
kuweka viongozi wake kwa masilahi binafsi badala ya wanaopendekezwa na wanachi.
Hata hivyo baada ya taflani
iliyodumu kwa takribani nusu saa Mwenyekiti Kisulu alizira kikao na kuondoka
zake akiwaacha wajumbe wamkutano huo wakiwa wamechachamaa wakishutumiana kwa
maneno makali yakiwemo ya ubaguzi wa uzawa na kushikana mashati.
Kumegeka kwa wana ccm
kulienda mbali zaidi baada ya wanachama kutoka Madesa kutamka wazi wazi kuwa
kama mgombea wao hata pita basi watakiua chama kwa kumchagu kiongozi kutoka
upinzani na hatakama atashinda mgombea wa chama hicho basi hawatashirikiana nae
hadi atakapoondoka madarakani.
“kwanza mgombea wenu
‘Madesa’ Eliazari Kaloli mmempitisha kwa rushwa,iweje kura ziwe nyingi kuliko
wajumbe wa mkutano halafu mnataka mmpitishe...tunasema akipita tunakiua ccm kwa
kuwaunga mkono upinzani”alisema Selemani Juma.
Huu ni mchakato kumpata
mgombea uenyekiti na wajumbe wa halamashauri ya kijiji ndani ya chama cha
mapinduzi CCM ikiwa ni hatua ya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe
4/12/2014 ambapo wateule katika chama hicho watakutanishwa na wateule wa vyama
vingine ili kumpata mwenyekiti.
No comments:
Post a Comment