MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday, 25 November 2014

DC PANGANI AWAJIA JUU WAKWAMISHA UJENZI WA MAABARA



·   MKUU wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa amesema kuwa hatamvumilia mtu yeyote atakaeonekana kukataa au kushawishi jamii kutoshiriki katika uchangiaji wa ujenzi maabara badala yake atamchukulia hatua kali za kisheria.

Mtasiwa ametoa kauli hiyo wakati akipokea msaada wa bati 200 yenye thamani ya shilingi milioni nne kutoka kwa Muko wa hiaadhi ya jamii PSPF ikiwa ni mchango wao wa kuunga zoezi la ujenzi wa maabara linaloendelea nchini kote.

Amesema kuwa katika wilaya hiyo kuna baadhi ya shule bado ujenzi unasuasua kutoka na wananchi kukosa ushawishi wa kuchangia ujenzi huo.

Nae Afisa mfawidhi wa mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF Salome Makala alisema kuwa wameamua kuchangia ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha elimu.

No comments:

Post a Comment