MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Monday 10 November 2014

BALOZI IDD AWAPA SOMO UVCCM

MAKAMU wa pili wa Rais wa Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi SEIF ALLI IDD ameitaka Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi UVCCM kutokubali kutumiwa au kugeuzwa ngazi ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mmwaka 2015.

Balozi IDD amesema hayo leo mjini Dodoma wakati akifunga baraza la UVCCM Taifa lililoanza juzi kama semina.

Amesema wakati wa kinyang'anyiro cha Urais unakaribia kufika hivyo wanapaswa kujihadhari wasije wakagawana mapande na kudhoofisha Jumuiya kwa sababu ya kuwaunga mkono wagombea fulani na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ameeleza kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania ni vijana hivyo wasije wakakukubali kutumiwa kutokana na uwingi wao.

Balozi IDD amesema umoja huo ni muhimili unaptegemewa na chama katika uhai wake kwenye ulingo wa siasa hapa nchini na kuyumba kwake ni kuyumba kwa CCM pia kwa kuwa vinana ndio benki ya wananchama na viongozi imara.

Akizungumzia kuhusu katiba  pendekezwa amewataka vijana wa CCM kujipanga vizuri kuendesha kampeni za kisayansi za kutafuta kura nyingi za ndio zitakazotoa ushindi wa kupitishwa kwa Katiba inayopendekezwa ambayo inayo maslahi makubwa kwa Chama na Taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhamasisha  wananchama pamoja na wananchi kwa ujumla kuipigia kura ya ndio.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa UVCCM Taifa ndugu SADIFA JUMA HAMISI  amesema Katiba pendekezwa ni lazima ipite kwa kishindo kizito katikakura ya maoni itakayopitishwa aprili mwakani kutokana na uundwaji wake mzuri ,maudhui na malengo yake.

Amesema kazi ya kuoata ushindi na kuipitisha katiba hiyo haihitaji kutegeana au kususiana bali inahitaji kufanywa wakiwa kitu kimojania ikiwa ni kufanikisha ushindi na kuwaangamiza maadui wanaotaka kuwavuruga kwa njia moja ama nyingine

Kikao hicho mbali na mambo mengine kimemteua balozi IDD kuwa naibu kamanda wa jumuiya hiyo kwa upande  wa Zanzibar huku  upande wa Bara akisubiri kuteuliwa baadae ambapo kamanda mkuu wa jumuiya hiyo ni mzee KINGUNGE NGOMBARE MWIRU.

No comments:

Post a Comment