MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Thursday 6 November 2014

DODOMA YAWA JIMBO KUU KATOLIKI LA SITA NCHINI



WAUMINI WA MADHEHEBU YA ROMAN KATHOLIKI [RC] JIMBO LA DODOMA WAKIWA KATIKA IBADA.

BABA MTAKATIFU Fransisco amelifanya jimbo katoliki Dodoma kuwa Jimbo Kuu  la sita nchini Tanzania.

Hata hivyo mara baada ya kulipandisha hadhi Jimbo katoliki Dodoma kuwa Jimbo Kuu amemteua Askofu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Katoliki mbulu kuwa askofu  Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma.

Kwa hivi sasa jimbo kuu teule litakuwa linasimamia  majimbo ya Kondoa na Singida.

Askofu Mkuu  Mteule Beatus Kinyaiya  alizaliwa tarehe 9 may 1957 Shimbwe Jimbo katoliki Moshi ambapo tarehe 5 Juni 1988 alipokelewa kwenye shirika la wakapuchini na tarehe 25 Juni  1989 alipewa daraja Takatifu la Upadre.

Aidha Askofu mkuu mteule mnamo mwaka 2006 aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo katoliki Mbulu  na alisimikwa tarehe 2 Julai  akishika nafasi ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza Yuda Tahadeus Ruwaichi aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo kwa kipindi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Jimbo katoliki  Dodoma imesema kuwa  maandalizi ya kusimikwa kwa askofu Mkuu mteule yanatarajiwa kuanza mapema.

No comments:

Post a Comment