WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
mheshimiwa BERNAD MEMBE ameutaarifu umma wa watanzania na dunia kwa
ujumla kwamba madai yaliyotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini
Marekani ya Environmental investigation Agency EIA hayana ukweli wowote.
Pia amekanusha madai yamkwamba serikali ya
Tanzania haijali na wala haichukui hatua dhidi ya wanaojishughulisha na
biashara haramu ya pembe za ndovu.
Akitoa tamko la serikali kuhusiana na shutuma
iliyotolewa na taasisi hiyo dhidi ya serikali ya Tanzania leo bungeni mjini
Dodoma mheshimiwa MEMBE amesema taarifa hizo zote ni za kupikwa na kuungwa
mkono ili kuchafua heshima ya Tanzania na heshima ya Taifa la China.
Ametaja sababu za kusema taarifa hizo ni za uongo
kuwa taarifa kama hiyo sio mara ya kwanza kutolewa iliwahi kutolewa mwaka jana
na mtoa taarifa ambaye ametajwa kuwa chanzo cha habari ni mtu mmoja ambaye
walimkuta barabarani na kuanza kumuuliza maswali ilhali sio sio mtumishi wa
bandari wala uwanja wa ndege.
Mbali na hilo amesema ziara ya rais huyo wa China
ilikuwa ya masaa 24 na programu yake ilianza mara tu alipowasili nchini kuanzia
saa 9 alasiri hadi saa 4 usiku kwenye dhifa ya Taifa na kuhoji hizo
shopping zinazoelezwa kufanywa na ujumbe wa rais huyo zilifanywa muda gani.
Mheshimiwa MEMBE amewataka watanzania kutokubali
upuuzi wa aina hiyo kwa kuwa Tanzania ni Taifa huru halichaguliwi marafiki wala
halirithishwi maadui na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo wa kidugu na
China na kwame hawarudi nyuma kutokana na maneno ya uwongo na uzushi.
Jana vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi
vilito habari kwamba ujumbe wa rais wa China uliokuja nchini mmiezi 18
iliyopita ulijihusishq na ununuzi wa pembe za ndovu nchini chnazo cha habari
kikiwa ni kutoka kwa Taasisi hiyo ya EIA.
No comments:
Post a Comment