· WATU 12 wamefariki na
wengine kadhaa 44 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugonga
garimoshi katika eneo la Kiberege Tarafa ya Mangula Wilaya ya Kilombero mkoani
Morogogro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro
Leonard Paulo amesema kuwa basi hilo Kampuni ya SUPER ALJABIR lenye Namba za
usajili T.725 ATD SCANIA BUS lililokuwa likiendeshwa na KASIM NDELA (35) mkazi
wa Morogoro, liligonga garimoshi lililokuwa likisafiri kutoka Mbeya kwenda Dar
es Salaam wakati dereva alipojaribu kuvuka reli.
Waliofariki ni pamoja na wanaume 6
wanawake 4 na wasichana wawili wenye umri kati ya miaka 5 na 6.
Hata hivyo Kamanda Paul amesema kuwa
majeruhi 24 wametibiwa na wameruhusiwa, ambapo 20 waliobaki kati yao ni
wanawake 15 wanaume wane na mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment