MKUTANO wa kumi na sita na wa kumi na
saba wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania umefanyika mjini Dodoma.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya
Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Mikutano
hiyo haikufanyika kwa wakati uliopangwa kutokana na kuwepo kwa bunge maalumu la
katiba.
Taarifa hiyo
imeeleza kwamba mikutano hiyo yote miwili sasa itafanyika kuanzia tarehe 4 hadi
28 mwezi huu.
Kazi
zitakazofanyika katika mikutano hiyo ni pamoja na Bunge kukaa kama Kamati ya
Mipango kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 94(1) na kupokea, kujadili na kutoa
maoni na ushauri kuhusu bajeti ya serikali, vyanzo vya mapato pamoja na
mapendekezo ya utekelezaji wake.
Aidha
kutakuwa na kusomwa kwa mara ya pili na hatua zake zote kwa miswada ya Sheria
ya Serikali ambayo ilikwishasomwa kwa mara ya kwanza katika mikutano
iliyotangulia; Muswada Binafsi wa Mbunge na Muswada Binafsi wa Kamati
Miswada
itakayosomwa kwa mara ya pili ni Muswada ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani wa Mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2013, Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi wa Mwaka 2014 na, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya
Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014.
Aidha,
kutakuwa na maswali ya kawaida kwa mujibu wa kanuni ya 39 (1) ambapo kwa
mikutano hii miwili yatakuwa 265 na maswali kwa Waziri Mkuu kwa mujibu wa
kanuni ya 38(1).
No comments:
Post a Comment