MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday, 25 November 2014

GALAWA:MARUFUKU KUFANYA MAZOEA KAZINI



·    MKUU wa Mkoa wa Dodoma Luteni Msataafu CHIKU GALAWA amewataka watumishi wa Halmashauri zote za mkoani Dodoma kuhama katika utendaji wa kimazoea wanapokuwa maofisini badala yake wafanye kazi kwa vitendo vinatakavyowanufaisha wananchi katika suala linalogusa maendeleo.

Agizo hilo amelitoa baada ya kusikiliza na kupokea taarifa ya Wilaya iliyosomwa na Mkuu wa wilaya hiyo mheshimiwa BETTY MKWASA  baada ya Mkuu huyo wa mkoa kwenda kujitambulisha kwa kukutana na wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo.

Amesema  watendaji wengi ndani ya halmashauri  walio wengi hawana ubunifu badala yake wanafanya kazi kwa mazoea utendaji ambao hivi sasa umepitwa na wakati.

Amesema wakati ni wao  sasa wa kubadilika katika kufanya kazi zao kwa kuwa wanatakiwa  kuhama kule walikozoea  ambako hakuna maendeleo yanayoweza kubadilika kwa mwananchi na kuweza kuifurahia serikali.

Awali mkuu wa wilaya ya bahi mheshimiwa MKWASA  akisoma taarifa kwa mkuu huyo wa mkoa amesema  kuwa katika wilaya yake pamoja na changamoto zilizopo pia wamefanikiwa kujiinua kimapato ikiwemo ya ufugaji na kilimo.

Amesema  kwa mwaka wa fedha 2013/20 14 katika Halmashauri hiyo ilikisia kukusanya jumla ya shilingi milioni 725.8 kama mapato yake ya ndani ambapo hadikufikia juni mwaka 2014 ilifanikiwa kukusanya shilingi milioni 504.4  sawa na aslimia 69 ya lengo.

Pamoja  na makisio hayo wilaya pia imefanikisha kufikia malengo yake katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu ya awali,msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa maabara ambapo vyumba 5 vimekamilika kati ya shule 28 zinazohitajika kujengwa vyumba hivyo.

No comments:

Post a Comment