- Yakwamisha maandalizi mradi usimamizi rasilimali za asili
MAANDALIZI ya mradi wa kuboresha usimamizi wa rasilimali za asili za bonde la Ziwa Nyasa yamekwama baada ya nchi ya Malawi kutoiambua Tanzania kama mojawapo ya nchi zinazomiliki ziwa hilo.
Akijibu swali bungeni mjini Dodoma waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi dr TITUS KAMANI amesema ziwa hilo la Nyasa
linamilikiwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na Msumbiji.
Amesema nchi hizo kwa pamoja katika mwaka wa 2010
zilikuwa katika maandalizi ya mradi huo ambayo yalikwama.
Amesema juhudi za kutafuta suluhu kuhusu mgogoro huo
zinaendelea katika ngazi za kimataifa.
Hata hivyo dr KAMANI amesema serikali inajenga
karakana ya kutengeneza boti za uvuvi eneo la Mbaba Bay ili kuwawezesha wavuvi
kupata boti imara kwa urahisi,kufanya uvuvi wenye tija na hivyo kujiongezea
kipato.
Dr KAMANI alikuwa akijibu swali la mbunge wa viti
maalum mheshimiwa CYNTHIA HILDA NGOYE aliyetaka kujua miradi inayotekelezwa na
serikali kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi katika vijiji vya kata za
Ngonga,Matema,Mwaya,Kijunjumela,Katumba na Songwe wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment