ASILIMIA 56 ya maji yanayozalishwa na kusambazwa na Mamlaka ya Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) yanapotea bila kulipiwa imeelezwa.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe
alipokuwa akifungua mkutano wa 15 wa Mamlaka ya maji mijini.
Maghembe
amesema upotevu huo wa maji umekuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa mamlaka
hiyo na hivyo kuikoasesha mapato.
Amesema
hivi sasa DAWASCO imekuwa ikipata mapato ya jumla ya shilingi. Bilioni 3.5 kwa
mwaka lakini endapo maji hayo yangekuwa yakiwafikia wateja wote wangeweza
kupata zaidi ya hapo.
Waziri
Maghembe amesema ni vyema sasa mamlaka zote nchini zikahakikisha kuwa maji
hayapotei na yote yanayozalishwa yanawafikia walengwa.
Amesema
ni muhimu kutafuta teknolojia ambayo itabaini upotevu huo wa maji mapema ili
kudhibiti maji na kuongeza mapato kwa mamlaka.
Amesema
kwa upande wa Jiji la Dar es Salaam Wizara ina mpango wa kuhakikisha kila mteja
anafungiwa mita ya maji kwa ajili ya kuhakikisha kuwa analipa maji kadri
anavyotumia.
Awali
akimkaribisha Waziri kufungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema
Nchimbi amesema ni vyema mamlaka zinzoambatana katika utuoaji wa huduma zikawa
zinashirikiana katika kutoa huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment