KITUO cha Kisasa cha Uchunguzi na
Matibabu ya magonjwa ya binadamu kinachojengwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma
UDOM kipo katika hatua za mwisho mwisho za ukamilishwaji.
Kituo hiki kitahudumia wagonjwa kutoka maeneo
mbalimbali ya mikoa ya jirani ya na mkoa wa Dodoma na kinajengwa kwa ufadhili
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa gharama ya shilingi Bilioni 36
ambazo zimetolewa na mfuko huo kwa silimia 100.
Akizungumza
na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria kongamano la Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli ya Dodoma mjini humo walipotembelea na
kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa
Mlacha Shaaban amesema “Kituo hiki kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya
uchunguzi na utafiti pia kitatoa wataalamu kutoka katika kitivo cha afya
cha Chuo kikuu cha UDOM.
Shaaban
amesema wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa wakifundisha
wanafunzi na kuhudumia katika kituo hicho, Kituo hicho kinatarajiwa kuanza
kutoa huduma ifikapo Januari 2015.
No comments:
Post a Comment