Sakata
hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni ya fedha na kwa muda mrefu
umezusha mjadala mzito katika bunge.
Katika
ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu
mwenyekiti Deo Filikunjombe, imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na
ufisadi katika mchakato wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa
fedha ungeweza kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi
ya viongozi.
Kamati
hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika kutokana na kashfa hiyo
kuwa ni mwanasheria, Waziri wa nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati
pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Ripoti
hiyo ilitokana na ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) ambayo ilianika ukiukwaji mkubwa wa taratibu wakati wa uchotaji
wa fedha hizo pia mahojiano na mkurugenzi mkuu wa Takukuru na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA).
Waziri
Pinda anadaiwa kuwa alijua kuwapo kwa ufisadi huo na matamshi yake kuwa fedha
hizo hazikuwa mali ya umma, wakati Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema
ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia kuagiza fedha hizo zitolewe
kwenye akaunti hiyo.
Waziri
Sospeter Muhongo amelaumiwa kwa kukosa kuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa
sakata hilo, huku naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa kulidanganya
Bunge.
Kashfa
nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa katika bunge nchini na kusababisha
viongozi kuwajibika wakiwemo Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond, EPA
na sasa hii ya ESCROW ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi
mapendekezo yake ya kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi
wengine.
No comments:
Post a Comment