MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday, 7 November 2014

MUSWADA SHERIA YA HABARI WAPIGWA DANADANA



SERIKALI imeendelea kupiga danadana katika kuleta bungeni muswada wa sheria ya habari na kusema utaletwa Februari mwakani badala ya mkutano huu unaoendelea.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kusini, Sulemani Bungara (CCM), aliyetaka kujua ni lini serikali italeta Muswada wa vyombo vya habari Bungeni ili kuondoa ukandamizaji unaoendelea.

Katika swali la msingi Mbunge huyo, ametaka kujua maelezo ya serikali kwa wananchi juu ya kufungwa vituo vya Televisheni na Redio vikiwemo vya Taasisi za kidini na sababu iliyofanya kuvifungua.

Amesema, serikali haijafungia kituo chochote cha televisheni  siku za karibuni.

Amesema vituo hivyo vilifungiwa baada ya kuthibitika kukiuka Sheria na kanuni za utangazaji baada ya kutangaza maudhui ya kiuchochezi na kuhatarisha uvunjifu wa amani ya nchi.

Nkamia, amesema kabla ya kuvifungia taratibu zote zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kupewa onyo mara kwa kadhaa, kuitwa na kuhojiwa mbele ya kamati ya maudhui.

No comments:

Post a Comment