· SERIKALI,
imezipiga marufuku Mahakama za Mwanzo kuamua mashauri ya kesi za Ardhi kwani
jukumu hilo ni la Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya.
Onyo
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki, wakati
alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama
(CCM), lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola
(CCM).
Mbunge
huyo ametaka kujua kwanini serikali isitoe kauli na tamko la kuwataka Mahakimu
wa Mahakama za Mwanzo kutopokea kesi hizo na badala yake izipeleke kwenye mabaraza
ya ardhi.
Pia
ametaka kujua ni kwani serikali isibebe mzigo wa kuwafidia watu waliopata
hasara kutokana na ucheleweshwaji wa kesi uunaofanywa na Mahakama hapa nchini.
Katika
swali la msingi, alitaka kujua sababu zinazopelekea kesi ikae Mahakamani zaidi
ya siku zilizowekwa.
Amesema,
kukomesha tabia ya mahakama za Mwanzo kuhukumu kesi la Ardhi serikali
itawasiliana na Makama za mwanzo ili ziweze kuchukua hatua stahiki katika jambo
hilo.
Kuhusu,
ucheleweshwaji wa kesi taratibu zinafahamika kwa wale ambao watakuwa na
sababu za msingi lakini mahakama zimekuwa haziahirishi kesi bia sababu yoyote
endapo itakuwa kusababu zimeeleweka kamati za mahakimu na za majaji wataweza
kufuatilia na kuchukua hatua.
No comments:
Post a Comment