Barua ya aliyekuwa Miss Tanzania
2014 Sitti Abbas Mtemvu aliyowaandikia Lino International Agency kuhusu uamuzi
wake wa kujivua taji hilo.
|
HATIMAYE
kampuni ya Lino International Agency imemvua taji aliyekuwa mrembo wa Tanzania
2014 (Redd’s Miss Tanzania 2014) Sitti Abbas Mtemvu kwa kosa la kudanganya umri
katika mashindano hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga
amesema kampuni yake imeamua kumvua taji hilo mrembo huyo ambaye ni mtoto
wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu.
Taarifa
zinadai kuwa mrembo huyo aliitumia barua kamati ya uandaaji wa Miss Tanzania
iliyoeleza uamuzi wake wa kuvua taji hilo.
Baada
ya kukabidhiwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014 Oktoba 11, siku chache baadae
Sitti alikumbwa na kashfa ya kudanganya umri baada ya kuonekana kuna utofauti
wa umri kati ya leseni na pasipoti yake. Taji
hilo litakabidhiwa kwa mshindi wa pili Lilian Kamazima.
No comments:
Post a Comment