· MTU
mmoja Jeremia Steven Mshana (54) mkazi wa Tangasisi Wilayani Tanga mjini amefariki
katika ajali iliyohusisha Gari NO.T.413 SCX aina ya SUZUKI CARRY aliyokuwa
akiendesha kugongana na gari mali kampuni ya Hajees yenye namba za usajili T.935
aina ya BUW YOUTONG BUS.
Imefahamika kwamba Hajeez ilikuwa
ikiendeshwa na Omari Nguku mwenye umri
wa miaka 38 mkazi wa Tanga Mjini wakati akitokea
Arusha kuja Tanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoani Tanga Frasser Kashai amesema
ajali hiyo imetokea mnamo Desemba 10 mwaka
huu majira ya saa 10:15 jioni eneo la Maguzoni
Kata ya Songa Tarafa ya Mbwembwela Wilaya ya Muheza. Marehemu alikuwa akitokea
Tanga kuelea Segera.
Aidha Chanzo cha ajali
hiyo ni kutokana na Dereva wa Bus kuhama
upande wake, na Kamanda Kashai amesema dereva huyo amekamatwa na atafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
No comments:
Post a Comment