MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Thursday 4 December 2014

WATANZANIA SAIDIENI YATIMA NA WALEMAVU

MSHAURI wa mradi wa kitaaluma kutoka nchini Finland Tero Tapani amewataka watanzania kuwasaidia, kuwajali na  kuwatahamini watoto yatima na walemavu kwani watoto wote ni sawa na wana nahaki ya kuishi kama wengine.

Tpani alikuwa akizungumza katika sherehe ya watoto yatima na walemavu ambayo imefanyika katika ukumbi wa mkutano YDCP Desemba 2, mwaka huu Jijini Tanga.

Amesema jambo bora na lenye Baraka ni kuwathamini watoto mlemavu na kuwatunza, kwani hata kristo aliagiza kuwaacha watoto waende kwake kwa kuwa kuna siri nyingi za ufalme wa Mungu.

Mratibu wa kituo cha YDCP, William Henry amesema kuwa lengo la kuadhimisha sikukuu hiyo ya watoto kila mwaka ni kuwaweka pamoja ili wajisikie vizuri kama watoto wengine.

Naye Mch. Ayubu Kuminambili wa kanisa la Free Pentekoste Of Tanzania (FPCT) ambaye alimwakilisha makamu Askofu wa kanisa hilo nchini Stivie Mulenga amesema kuwa amdharauliye wenzake atenda dhambi bali amhurumiaye mwenzake ana heri, hivyo ni vyema kuwapenda watoto walemavu na kuwatunza kwani Mungu amewaumba kwa makusudi maalum.

No comments:

Post a Comment