SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Idara ya Kuondoa Umaskini inaandaa
kongamano la kimataifa linalohusu kinga ya jamii litakaofanyika jijini
Arusha kuanzia Disemba 15 hadi 17 mwaka huu.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile wakati wa kikao cha wataalam wa sekta na waandishi
wa habari kuhusu kongamano hilo.
Dkt.
Likwelile alisema kuwa Mgeni Rasmi atakayefungua kongamano hilo
anatarajiwa kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete na unatarajiwa kufungwa na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda.
Kongamano
hilo litahusisha watunga sera, watafiti na watu wanaojihusisha moja kwa
moja kwenye kubuni, kupanga na kutekeleza programu za kinga ya jamii na
mifumo yake kwa kwa lengo la kubadilishana ujuzi na uzoefu.
Dkt.
Likwelile alisema kuwa majadiliano katika kongamano hilo la siku tatu
yatalega kuwajengea washiriki uelewa zaidi juu ya kinga ya jamii na
matumizi yake kwa sera, programu na utawala pamoja na kushirikiana
katika kutumia matokeo ya tafiti, masuala ya kujifunza na namna bora ya
kuandaa na kutekeleza programu na mifumo inayohusu kinga ya jamii.
Malengo
mengine ya kongamano hilo ni pamoja na kuainisha mambo ya msingi
yanayohusu kinga ya jamii ambayo yanahitaji kuchukuliwa na kuingizwa
kwenye agenda kuu ya kinga ya jamiii kwa ajili ya maendeleo ya usoni na
kuandaa uwanja wa kubadilishana uzoefu na hatimaye kuwa na mikakati
mizuri ya pamoja inayohusu kinga ya jamii.
Nchi
zitakazoshiriki kongamano hilo linaloandaliwa na Serilkali ya Tanzania
kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS NA EPRI ni Kenya, Uganda,
Bangladesh, Afghanistan,Msumbiji, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana,
Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment