UCHAGUZI
wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika jana nchini ulitawaliwa
na dosari ambapo Mkoani Tanga katika baadhi ya maeneo yamelazimika kuahirisha zoezi
la upigaji kura hadi DEC 21, 2014.
.jpg)
Mkurugenzi wa Jiji la
Tanga, Juliana Malange amezungumza na Mwanamkemakini juu ya sababu
zilizosababisha kutofanyika uchaguzi huo kuwa ni kasoro zilizojitokeza kwenye
karatasi za kupigia kura.
Aidha taarifa ya
matokeo kwa maeneo walio piga kura ambapo CCM kwa nafasi ya mwenyekiti mitaa 118,
CUF mitaa 60, Chadema mitaa 2, kwa nafasi ya Wajumbe mchanganyiko CCM 356, CUF 117
na Chadema 3, Vitimaalumu CCM 230, CUF 162 na Chadema 2.
“Katika uchaguzi huu
kwa nafasi ya mwenyekiti CCM ilishinda kwa 65%, CUF 33% na Chadema 1%.
No comments:
Post a Comment