·
JESHI la Polisi Mkoani Tanga linatoa shukrani kwa wananchi kwa kutoa
ushirikiano mzuri wa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu
kipindi hiki cha Krismas na hivyo kuwezesha wananchi kusherehekea kwa amani na utulivu .
Akitoa taarifa ya hali ya uhalifu kwa waandishi wa habari
akiwa ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Frasser Kashai
amesema wanawaomba wananchi kuendeleza ushikiano huo ili kuweza kuvuka salama
mwaka 2014 kwa amani.
Aidha Kamanda Kashai amesema kutokana hali ya uvunjivu wa
amani kuendelea kuijtokeza katika maeneo mbalimbali mkoani hapa kumekuwa
matukio yaliyojitokeza baadhi ya Wilaya za mikoa .
Amesema watu wawili
wamefariki katika matukio mawili taofauti ,ambapo amesema mnamo tarehe 26
majira ya saa moja kamili asubuhi huko maeneo ya Ndekai Kata ya Baga Tarafa ya Mgwashi Kando ya barabara ya Baga
–Kwemakame Wilaya Lushoto ,Mtu aliyefahamika kwa jina la Rshidi Kilua mwenye umri wa miaka mkazi wa Ndekai
,aligundua mwili wa Mpwa wake aitwe Hashimu
Rajabu ukiwa na majereha kichwani
.
Hata kamanda amesema mwili marehemu umefanyiwa uchunguzi na
madaktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.
Amesema chanzo cha mauaji hayo kinasakiwa kuwa ni Migogoro ya
ardhi ,ambapo mpaka sasa watu wawili
ambao ni Waziri Salimu umri wa miaka 35 mkazi wa Ndekai Baga wapili ni Ramadhani Ayub umri wa miaka 40
mkazi wa Mwangoi Baga wamekamatwa
kufauati mauaji hayo kwa ajili ya mahojiano .
Katika tukio njingine kama hilo Mtun mmoja aliye fahamika kwa
jina la Husein Muamed amefariki Dunia wakati alipokuawa anapata matibabu katika
Hospitali ya Bombo mara baada ya kokolewa wakati alipokuwa akishambuliwa na
wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za uwizi baada ya kuvunja
nyumba na kuingia ndani kwa nia ya kuiba .Kamanda Kashai amesema upelelezi unaendelea kufuatia tukio
hilo ili kuwabaini waliojichukulia
sheria mkonani.
Katika hatua nyingine jeshi la Polisi mkoani hapa
linawashikilia watu wapatao sita ambao
ni ni Raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia Nchini bila kibali .
Kamanda Kashai amewataja watuhumiwa hao kuwani Gesamu Abato
mwenye umri wa miaka 30,Hash Negash Grinanu umri wa miaka 20,Tsegaye Aliso umri
wa miaka 21 ,Jamal Godso umri wa miaka
25 ,Alemayo Ataro umri wa miaka 22 na Erigudo Elitiro umri wa miaka 25 .
Kamanda Kashai amesema Watuhumiwa hao watafishwa mahakamani baada
ya upelelezi wa awali kukamilika .
No comments:
Post a Comment