MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday 16 December 2014

ASKARI WALIOSIMAMIA UCHAGUZI MDOGO TANGA BADO HAWAJALIPWA



ASKARI Mgambo wapatao 200 wameilalamikia ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kwa kutowalipa fedha zao kama malipo kwa kazi ya usimamiaji zoezi la kupiga kura.

Baadhi ya askari hao MG 427805, MG 351976 na MG 265079 wakizungumza na Redio Huruma kwa niaba ya wenzao walipofika ofisi za Jiji la Tanga wamesema licha ya kuelekezwa kumfuata Mkurugenzi Juliana Malange ili awezeshe malipo hayo zaidi ya mara mbili juhudi zao zimegonga mwamba bila kupatiwa majibu ya kina.

Mwandishi wetu Rebecca Duwe alizungumza na Mkurugenzi kwa njia ya simu ambeye naye aliyolea ufananuzi huu suala hilo kuwa yeye siye aliwewapangia vituo hivyo itamuwia vigumu kuwatambua.

Ameongeza kwamba ni vyema wakawasiliana na OCD ambaye atawasilisha majina kwane ili aweze kukamilisha hayo malipo kwasababu fedha zipo kwa ajili ya kufanya hivyo.

Hata hivyo wenzao (waalimu) tayari walipatiwa malipo yao hata kabla ya zoezi kuanza.

No comments:

Post a Comment