WAKATI Taifa likisherekea
siku kuu ya TISA DESEMBA Gari yenye namba za usajili T.131 AZZ SCANIA
mali ya kampuni ya Saibaba limekamatwa likiwa na raia 12 wa
Ethiopia likiwasafirisha kutokea Arusha kuelekea jijini Dar es salaam.
|
Raia hao wamekamatwa majira ya saa
10:30 jioni maeneo ya Mbwiko Kata ya Mbwiko Tarafa ya Mombo barabara kuu ya
Mombo –Segera Wilayani Korogwe.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Tanga, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Frasser kashai amewataja raia hao
kuwa ni Kashoma Bayen umri wa miaka 24,Berchano Gamada umri wa miaka 32, Awal
Jamal umri wa miaka 23 ,Yanis Gatiso umri wa miaka 28, Metson
Sipril umri wa miaka 21,Tashona Hayalis umri wa miaka 30.
Wengine ni Adino Samiru umri wa miaka
20, Kengeny Siyun umri wa miak 22 ,Charnes Egesa umri wa miaka 20, Abdi
Bandru umri wa miaka 21, Siumanda Siumanda umri wa miaka 26 na Na Malako Abuu
umri wa miaka 23.Watuhumiwa wote watakishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayowakabili.
MTOTO NAE KINAWA WA BIASHARA
|
Hawa walikamatwa siku za nyuma nchini |
Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Ally Mbukuzi mwenye umri wa miaka 17 mkulima na mkazi wa Putini kata ya
Chongoleani Wilaya ya Tanga kwa kosa la kuwaasafirisha wahamiaji haramu wapatao
sita (6) ambao ni Raia wa Ethiopia.
kamanda Kashai amesema kuwa mnamo
tarehe 8 Disemba mwaka huu majira ya saa saba 13:00 mchana, huko katika
kisiwa cha Jambe Kata ya Tongoni Tarafa ya Pongwe Wilaya Tanga wamekamatwa
Dolec Dalalo umri wa miaka 28, Alaleus Tesame umri wa miaka 21,
Hashinavia Shamibu umri wa miaka 23, Taken Ndasalh umri wa miaka 20,Tamesgen
Kisfon umri wa miaka 20, Mihon Eriamin umri wa miaka 22.
Aidha mtuhumiwa amekiri kufanya kufanya
biashara hiyo ya usafirishaji wa wahamiaji haramu na atafikishwa mahakamani
mara baada ya upelelezi kukamilika.
ONYO KALI
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linatoa onyo
kali kwa watu wanaovunja Sheria ya Kuingiza wahamaiaji haramu kinyemela
ndani ya nchi kinyume cha sheria. Jeshi la polisi litawafuatilia watu hao na
kuhakikisha kwamba wanakamatwa pamoja hamaiaji hao haramu ambao
wanawasafirisha.
Aidha amewashaukuru wananchi kwa juhudi
za kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuwapa ushirikiano juu ya
uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo yao wanayoishi.
Pamoja na hayo aliwasisitizia wananchi
kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao wanayoishi ili
kuweza kuzuia na kukabiliana na uhalifu mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment