MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday, 12 December 2014

MCHUNGAJI AKEMEA WANAOITA WATOTO MCHUMBA, ASEMA NI UDHALILISHAJI



KIONGOZI wa Kanisa la KKKT Pemba Mchungaji Benjamini Kisanga amekemea tabia ya baadhi ya wazazi kuruhusu watoto wa Kike kuitwa mchumba hali ambayo inachagia kuwepo na matendo ya udhalilishaji wa Kijinsia.

Amesema kuwa kuruhusu mtoto wa kike kuitwa mchumba kunawajengea mazingira ya kuwazoea watu na hivyo kuwa ni rahisi kwa mtoto huyo kudhalilishwa.

Akizungumza na redio Huruma Kisiwa Pemba  kwenye maadhimisho ya haki za Binadamu , ameitaka jamii kuwalinda watoto wa kike kwa kuhakikisha kwamba wanakemea vitendo vya kuitwa mchumba.

Aidha Mchungaji huyo wa kanisa la KKKT amesema baadhi ya watu wanatabia mbaya na hivyo wanapata mwanya wa kutekeleza matendo hayo baada ya wazazi kukubali  watoto wao kuwa na mazoea na watu.

Hata hivyo ameishauri jamii kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kuwalinda na makundi maovu ambayo ynaweza kuwa ni kishawishi cha kuharibu mustakabali wa maisha yao.


No comments:

Post a Comment