ALIYEKUWA Mkuu wa mkoa Tanga Chiku Gallawa ambaye kwa sasa ni Mkuu wa
Mkoa Dodoma amewaomba wakazi wa mkoa wa Tanga kutoa ushirikiano mzuri na
kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa mpya ambaye ameletwa Tanga baada ya mabadiliko ya
wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais.
Katika
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilitoa maelekezo ya Mkuu Magalula Saidi
aliyekuwa Mkoa Katavi kuja Tanga.
Alizungumza hayo wakati wa makabidhiano ya majukumu ya kazi baina yake na mkuu huyo
mbele ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na waandishi wa
habari katika ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Kwa
upande wake Mkuu wa sasa wa Mkoa wa Tanga Magalula saidi amewasihi wananchi
kuendeleza kazi iliyoachwa na Galawa kwa mustakabali wa maendeleo ya wana Tanga.
No comments:
Post a Comment