TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imeanza kazi ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura.
Katika
maboresho hayo, tume imeanzisha mfumo wa kuchukua au kupima taarifa za mwili au
tabia ya mtu ujulikanayo kama Biometric Voter Registration, BVR na kuzihifadhi
kwenye data base za tume hiyo.
Vyama
vya siasa na wadau wengine wa masuala ya uchaguzi wamekuwa wakitaka pawe na
mfumo utakaosaidia kuondoa udanganyifu unaosababisha uchaguzi kutokuwa huru na
wa haki.
No comments:
Post a Comment