Marekani
imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la
Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya
Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.
Haya
yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo
yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh.
bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo.
Katika
tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza
kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko
lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua
za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la
suala la IPTL.
Taarifa
iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ilieleza kuwa wakurugenzi wa
MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu
wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.
Itakumbukwa Wakati wa mkutano wa 16 na
17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza
kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment