MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Sunday 28 December 2014

MAHAKAMA YADAIWA KUITESA FAMILIA YA WATU 18 MOROGORO



  FAMILIA ya watu 18 wakiwemo watoto 10 na akina mama Nane mtaa wa Juma 50 kata ya Mwembesongo eneo la Mafisa Msamvu Kilabu cha Makondeko Manspaa ya Morogoro wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko na uambukizo baada ya kutupiwa vitu vyao nje ya nyumba kwa madai ya amri ya mahakama.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani  hapo, baadhi ya wanafamila hao Magreth Kainyingi  na Adistela Kainyingi walisema tukio hilo walichofanyiwa Desemba 23 limelenga kuwadhalilisha,kuwafedhehesha na kuwadhoofisha kimaendeleo kwakua hapo ni kwao kihalali.

Walisema chimbuko la mgogoro huo ni deni wasilolitambua la shilingi 800,000 walilokopeshana kati ya baba yao na mtu waliemtaja Josia Masini aliebadili dhana ya mkopo nakuwa malipo ya ununuzi wa nyumba hiyo.

Katika ufafanuzi huo Magreth alisema mbali na vielelezo vya hati miliki walivyonavyo katika eneo hilo Ploti namba 35 kitalu ‘A’Msamvu,na kuthibitishwa na vyombo vya usimamizi ikiwemo Manspaa bado Mahakama imekuwa ikipinga uhalali wake na kumpatia haki Masini.

Wakizungumzia kutupwa nje kwa mizigo yao walisema Desemba 23 walivamiwa na watu wasiowajua waliojitambulisha kuwa wafilisi wa mahakama kisha kuanza kubeba mizigo na kuitoa nje huku wakiwataka kulipa shilingi 900,000 kama usumbufu.

Kwa nyakati tofauti imefikia Masini akishirikiana na uongozi wa mtaa amekuwa akiwakamata kuwafikisha polisi na mahakamani na tayari alishawahi kuwafunga jela mwaka mmoja na kazi ngumu wakiwa na watoto wadogo.

No comments:

Post a Comment