WIZARA
ya afya na Ustawi wa Jamii imetoa tunzo ya BIMOC kwa Kituo cha afya cha Pongwe
pamoja na vyeti maalum vya daraja la kwanza.
Akifafanua maana ya
BIMOC katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo hii leo mganga mkuu Faisal
Ally, mara baada ya kupokea tunzo hiyo amesema hiyo ni kuonyesha kuwa kituo
hicho ni bora kwa huduma ya mama na mtoto
Sanjari na hayo pia
Mganga huyo ameelezea uwezo mwingine walionao kituoni hapo kama vile kufanya
upasuaji, kutoa dawa za usingizi, huduma ya kutoa na kuhifadhi damu salama
ambayo wanategemea kuianza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa mahitaji ya
vifaa kadhaa.
Hata hivyo changamoto
inayowakumba katika kutoa huduma kwa mama wajawazito ambayo hutolowa bure ameelezea
kuwa ni urejeshaji wa matumizi wanayotumia kuwahudumia
No comments:
Post a Comment