MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Thursday 27 November 2014

AJALI YAUA 13 TANGA, WAMO INSPECTER WA POLISI NA SISTER WA ANGLICAN



WATU 13 wamethibitishwa kufa na wengine 19 kujeruhi baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ''Thende Sheki'' yenye namba za usajili T 410 BJD kugongana uso kwa uso na lori la mizigo Scania namba T 605 ABJ katika eneo la Mkanyageni lililopo wilayani muheza.
 
Katika ajali hiyo, iliyotokea majira ya saa 1:30 asubuhi ya leo Coaster lilikuwa likitoka mkoani Tanga kuelekea wilayani Lushoto likiwa limepakia abiria 27.
 
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema dereva mwenye lori alikuwa akiyumba njia nzima kabla ya kukutana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Coaster hatua waliyodaiwa kuwa dereva huyoo alikuwa amepitiwa na usingizi.

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Juma Ndaki amethibitisha ajali hiyo na kuwataja madereva kuwa ni wa Coaster Bakari Mussa amevunjika mkono wa kulia na wa Scania Banjamini Abeli ameumia kichwa na miguu.

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni Sister Hellena wa Kanisa la Mt Augustino Anglican Chumbageni, Salumu Hussein (30), Muddy Mohamedi (35), Ahmed Shemdoe (48), Julius Manyama (60), Zawad Juma (35), Frida Benjamini ambae hakufahamika umri mara moja.

Wengine ni Inspecta wa Polisi wilaya ya Muheza Antony Masanya, Kadiri Alfani (29), na wengine majina yao bado hayajatambuliwa.

No comments:

Post a Comment