SERIKALI imeingia mkataba na kampuni ya simu ya
Viettel kujenga mawasiliano katika vijiji elfu 10 kwa kuanzia.
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia
mheshimiwa MAKAME MBARAWA amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu
swali la nyongeza la mbunge wa Kilwa Kaskazini.
Katika swali lake mheshimiwa MANGUNGU ametaka kujua
mkakati wa serikali katika kuondokana na tatizo la mawasiliano nchini.
Mheshimiwa MBARAWA amesema kwa kuanza kampuni hiyo
itaanziana vijiji elfu 4 kuanzia sasa mpaka mwezi octoba mwakani.
Aidha kuanzia octoba mwakani hadi octoba mwaka kesho
kutwa vijiji elfu 2 vitapatiwa mawasiliano ikifuatia vijiji elfu 1 mia 8 na
kumalizia vijiji elfu 1 mia 2.
No comments:
Post a Comment