MZEE wa 70 Frorida Msanga mkazi wa Saruji amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari wakati akitembea kwa mguu maeneo ya Kiwanda cha saruji kata na Tarafa ya Pongwe Wilaya ya Tanga.
Ajali hiyo ya Novemba 15 mwaka huu imetokea majira ya saa 1:45 usiku ambapo gari aina ya Toyota mark II lenye namba za usajili T.454 BCG lilikuwa likiendeshwa na Morisi Daffa 49 mkazi wa Sahare Tanga alimgonga
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna mwandamizi msaidizi wa Polisi Fresser Kashai amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hiyo kuendesha mwendo kasi huku akiwa amelewa.
Hata hivyo kashai amesema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment