MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Wednesday, 19 November 2014

SOKO LA SAMAKI WILAYANI MUHEZA LAANGUKA, WAFANYA BIASHARA ZAIDI YA 50 WAKOSA ENEO LA KUFANYIA BIASHARA

SOKO maarufu la samaki wilaya ya Muheza limebomoka na kusababisha majeraha kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Kaoneka ambae amepatiwa matibabu katika hospitali teule wilayani humo na hali yake inaendelea vyema

 Soko hilo ambalo lipo chini ya halmashauri licha ya wafanya biashara kutozwa ushuru lilikuwa likikabiliwa na uchakavu wa miundombinu kutokana na kujengwa zaidi ya 20 iliyopita. 

Kwa sasa zaidi ya wafanya biashara 50 wamekukosa maeneo ya kufanyia biashara yao. 

Wakizungumza na mwananamkemakini aliyefika kushuudia tukio hilo wafanyabiashara wa sokoni hapo wamesema kuwa ahadi ya halmashauri ilikuwa ni kulifanyia ukarabati baada ya ujenzi wa soko la sakura kukamilika ahadi ambayo hata hivyo haikutekelezwa.

No comments:

Post a Comment