WAZIRI
wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa BERNAD MEMBE
amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijapata taarifa zozote
rasmi kutoka Jamhuri ya Kenya kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya serikali hizo
mbili.
MEMBE amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge
baraza la wawakilishi mheshimiwa JAKU HASHIM AYOUB.
Katika
swali lake mheshimiwa JAKU ametaka kujua serikali inasema nini juu ya taarifa
iliyoripotiwa na vyombo vya habari kuwa kisiwa cha Pemba ni sehemu ya Kenya
kufuatia mgogoro wa mpaka uliojitokeza kati ya Kenya na Somalia kuhusu vitalu
vya mafuta.
Mheshimiwa
MEMBE amesema kisiwa cha Pemba ni sehemu ya Jamhuri ya Muungnao wa
Tanzania na kitanedelea kubakia hivyo daima na kwamba watatoa maelezo zaidi
endapo tu itapokea madai hayo kutoka serikali ya Kenya.
Amesema
baada ya wizara kupata suala hilo waliwasiliana na balozi wa
Tanzania nchini Kenya na serikali ya Kenya lakini wote walikuwa hawaelewi
suala hilo limetokea wapi ila wanachofanya ni kusubiri kwa sabahu uongozi sio
serikali peke yake inawezekana ilianzia kwa watu binafsi,asasi za kiraia au
mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mheshimiwa
MEMBE amesema serikali inawaomba wananchi hususan waishio katika
Kisiwa cha Pemba kutokuwa na hofu yoyote juu ya maai kuwa kisiwa hicho ni
sehemu ya Kenya na waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa kama kawaida.
MWISHO.
DODOMA
KUTOKANA
na kukithiri kwa tatizo la Ujangili nchini serikali imezindua Mkakati wa
Kitaifa wa Kupambana na Ujangili wa mwaka 2014 hadi 2019.
Katika
mkakati huo watatoa mwongozo kwa wadau wa uhifadhi ndani ya nje ya nchi
kushiriki katika mapambano dhidi ya ujangili.
Akijibu
swalileo bungeni mjini Dodoma naibu waziri wa Maliasili na Utalii mheshimiwa
MAHMOUD MGIMWA amesema kwacsasa wizara imechukua hatua mbalimbali za
kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuajiri wahifadhi wanyamapori 437 kwa ajili
ya kuimarisha doria dhidi ya ujangili.
Aidha
wametoa mafunzo na vitendea kazi kwa watumishi na elimu ya uhifadhi kwa jamii.
Mheshimiwa
MGIMWA alikuwa akijibu swali la mbunge wa Dole mheshimiwa SYLVESTER MABUMBA
aliyetaka kujua mikakati iliyochukuliwa ili kukomesha tatizo la ujangili
nchini.
Katika
swali la nyongeza mbunge wa Same Mashariki mheshimiwa ANNE KILANGO ametaka
kujua sababu ya serikali kuendelea kuruhusu uwindaji ilhali imekiri
kuwepo kwa tatizo la ujangili.
Akijibu
swali hilo mheshimiwa MGIMWA amesema suala la kuruhusu uwindaji ni masuala ya
kimkataba hivyo wanangoja wapate ushauri kutoka ndai ya bunge na wao
watalifanyia kazi.
MWISHO.
DODOMA
JUMLA
ya miradi ya uwekezaji elfu 3,683 imesajiliwa katika kipindi cha mwaka 2010
hadi octoba 2014.
Kati
ya miradi hiyo miradi elfu 1,872 sawa na asilimia 51 nimiradi ya
wawekezaji wa ndani,miradi 948 sawa na asilimia 26 ni miradi ya ubia kati ya
kati ya wawekezaji wa ndani na nje.
Hayo
yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu
uwezeshaji na uwekezaji mheshimiwa MARRY NAGU wakati akijibu swali la
mbunge wa viti maalum mheshimiwa RITA MLAKI.
Katika
swali lake mheshimiwa RITA ametaka kujua serikali inaeleza nini bunge kwa
kipindi cha miaka minne tangu kuwekwa ka wizara hiyo kuwa ni wawekezaji wangapi
wameingia nchini na wamesaidia kukuza uchumi kwa kiasi gani.
Mheshimiwa
NAGU amesema manufaa yanayoambatana na uwekezaji huu ni pamoja na kuongezeka
kwa ajira zaidi ya laki 5,kuingizwa mitaji mikubwa,kuongezeka mapato ya serikali
kupitia kodi mbalimbali zitokanazo na miradi ya uwekezaji na kupata teknolojia
za kisasa.
Amesema
serikali imeendelea kuhamasisha wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi
kuwekeza hapa nchini kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa Tanzania.
MWISHO
No comments:
Post a Comment