HALMASHAURI ya Jiji la
Tanga imesema litachukua maamuzi magumu kwa ajli ya kurekebisha
suala la ugawaji wa fedha ambayo hutolewa na kila halmashauri kwa ajili
kukamilisha ujenzi wa maabara kwenye kila shule ndani ya kila kata ikiwa ni utekelezaji
wa agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo ameyafahamisha Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Omari
Guledi katika kikao cha kamati za Halmashauri ambazo huwashirikisha madiwani 24
wa kata ndani wilaya Tanga kilichofanyika katika ofisi za mipango miji mjini
hapa.
Aidha kutokana na baadhi ya kata kukosa haki hiyo ya kupewa fedha
ya ujenzi wa Maabara tatu kwa mwaka huu, Guledi amesema Halmashauri itahakikisha
fedha hizo zinawafikia ili ujezi huo ufanyike kwa maslahi ya wananchi wote wa
Tanga.
Hata hivyo baadhi ya madiwani wametaka maamuzi hayo yasiegemee
kwa baadhi ya kata na kwamba kila kata ambayo haijaingiziwa fedha zake
kikamilifu wapatiwe haki zao huku wakipigia upatu maabara katika shule za vijijini
zipewe kipaumbele kwani zimeonekana kusahaulika sana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Bi.Juliana
Malenge amewatoa hofu madiwani wote hususani ambao hawajapokea fedha za ujenzi
wa maabara na madarasa kuwa mara utaratibu ukikaa vizur,i maamuzi hayo yatatekelezwa.
No comments:
Post a Comment