BUNGE limeelezwa kuwa upungufu wa Dawa na ukosefu wa ajira hapa nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa takwimu.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi Viwanda na Biashara Luhaga Mpina
alipokuwa akitoa maelezo ya kamati kuhusu Muswada wa Sheria ya Takwimu ya 2013.
Mbunge Mpina amesema
kukosekana kwa takwimu kunachangia hali hiyo kutokana na kutokuwepo kwa tafiti
na taarifa sahihi zinazowaongoza wanafunzi kuchagua na kusomea fani kulingana
na mahitaji ya soko la ajira na vijana wengi kukosa ajira.
Amesema hivi sasa hakuna takwimu
halisi za wagonjwa wanaokufa kwa kukosa matibabu na ndiyo maana maamuzi kama ya
kulipa deni la MSD yamekuwa yakisuasua.
Mpina amesema uzoefu umeonyesha kuwa
nchi zote ziliopiga hatua kubwa kimaendeleo zina mifumo imara ya upatikanaji wa
takwimu ambazo zinasaidia kupanga mipango ya muda mfupi, wa kati na mirefu.
Awali akisoma muswada huo
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum amesema madhumuni ya muswada huo ni kuipa
mamlaka zaidi Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kutekeleza majukumu ya kitakwimu kwa
uhuru na ufanisi.
No comments:
Post a Comment