MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Friday, 28 November 2014

KABLA YA SAA 24 KUPITA UNAHAKI YA KUJUA HAYA JUU YA ESCROW

WASIRA AFUNGUKA YAKE ASEMA HADI WATU KUBEBA FEDHA KWENYE LUMBESA HAKUNA NCHI HAPA!
Wasira: CAG sio mara ya kwanza kuchunguza na kuleta taarifa bungeni, na PAC nao hii ni kazi yao kuchunguza na kuleta Bungeni
Wasira: Jambo la pili ni wajibu sasa wa Bunge hili kutazama ripoti hizi na kuzifanyia kazi.
Wasira: Kama kuna mtu anataka kuwa Rais na mbinu zake ni kuondoa wengine huyo hafai kabisa kuwa Rais wa Tanzania
Wasira: Sisi bunge hili lazima tunangalie maslahi ya Watanzania, hatuwezi kutumiwa na mtu.
Wasira: Afadhali kuwa maskini mwenye heshima kuliko tajiri anayetukanwa
Wasira: Tutakuwa Bunge la ajabu kama maneno haya yameandikwa na vyombo hivi vya Bunge halafu sisi tukalifumbia macho.
Wasira: Nchi ambayo unaenda na sandarusi, mabox kubeba hela, hapa hatuna nchi, inabidi TAKUKURU watutajie ni kina nani hawa
Wasira: TAKUKURU iwachambue watu wote bila kujali vyama au nini ili tuwapeleke kwenye sheria
Mwandosya: Suala hili linatuondolea sifa kama nchi, linatuondolea heshima kama taifa, kimataifa na mbele za wananchi

HALIMA MDEE NA MNYIKA WAFUNGUKA YA KWAO JUU YA ESCROW
Bunge limekutana tena sasa na msemaji wa kwanza aliyekaribishwa ni @jjmnyika
jjmnyika : Utata uliokuwepo juu ya kifo cha Mh. William Mgimwa aliyekuwa Waziri wa fedha, wengine wakausisha kifo kile na ulaji wa fedha hizi za Escrow
Mnyika: Muhongo lazima awajibike kwa kujizuru na lazima awajibike kwa wananchi
Mnyika: Linapokuja suala la uwajibikaji kwa Mawaziri wa kawaida linaonekana sawa ila inapokuwa Waziri Mkuu mnamkingia kifua
Mnyika: Kama mtakumbatia hili suala tutachukua hatua za kupiga kura juu ya kukosa imani na Waziri Mkuu:
halimamdee : Mwanasheria Mkuu unatakiwa utupishe uende Tarime ukapumzike
halimamdee : Tukirogwa tukianza kudai kodi manaake ni kwamba serikali tumehararisha wizi huu
halimamdee : Mahakama kuu ya Tanzania haikuwa na mamlaka yoyote kushughulikia fedha za ‪#‎TegetaEscrow‬

KIGWANGALLAH ASEMA KUWA HAJAWAHI ONA PROF MUONGO KAMA WAZIRI MUHONGO
hkigwangalla : Wana CCM wenzangu itakuwa jambo la ajabu sana kama tutajiunga kuwa genge la kutetea uovu.
Ukisoma ripoti ya CAG kwa umakini hizi dhana zote za Mh. Muhongo ni uongo mtupu.
Kigwangallah: Muhongo ni mzoefu wa kusema uongo, mimi binafsi sijawahi kuona Prof. MUONGO kama huyu Prof Muhongo.
Kigwangalla: Ripoti zote alizotoa huko nyuma ni uongo hata jana amesimama na kusema uongo
hkigwangalla: Toka lini CAG akaenda kukagua fedha za mtu binafsi
Toka lini fedha za mtu binafsi zikakaa benki kuu?

No comments:

Post a Comment