MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Saturday, 8 November 2014

Y.W.C.A YAFANYIA USAFI SOKO KUU DODOMA



 
SHIRIKA la Y.W.C.A kupitia mradi wake wa wajibika leo limefanya Oparesheni maalumu ya usafi katika soko la majengo lililopo mjini Dodoma lengo likiwa ni kuhamasisha jamii ipende kujishughulisha na usafi wa mazingira.

Akizungumza na blog hii leo afisa miradi wa Shirika hilo bibi Bulalo Mtobesya amesema kuwa Shirika lake litaendelea kuhamasisha jamii ili iweze kufanya shughuli za usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.
Amesema kuwa shirika la Y.W.C.A kupitia mradi wake wa wajibika tayari limeunda klabu mbili za vijana katika shule ya mkonze sekondari pamoja na shule ya msingi Mlimwa B lengo ikiwa ni kurithisha vijana wapende mazingira na kupambana na vitndo vyote vya uharibifu wa mazingira.

Amesema kuwa Shirika la Y.W.C.A linajishughulisha pia na Vikoba,ufuatiliaji wa rasilimali za umma pamoja na maswala ya ujasiriamali.

Shirika hilo leo liliandaa mdahalo ulihusisha wadau mbalimbali ambao ulifanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea.

No comments:

Post a Comment