· SERIKALI ya mkoa wa Morogoro
na wadau wengine akiwemo Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam John
Guninita wamewagia misaada mbalimbali zikiwemo fedha tasilimu majeruhi wa ajali
ya Basi kuigonga Treni katika hospitali ya Mt.Francis wilayani humo.
Katika
misaada hiyo ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa pole kwa majeruhi 14 kila mmoja
walipata shilingi 50,000 huku majeruhi ambae hali yake haikuwa nzuri
alipewa shilingi 200,000 ili zimsaidie kuhamishiwa hospitali kuu ya rufaa
Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mbali
na fedha tasilimu katika misaada iliyotolewa, misaada mingine ni pamja na maji
ya kunywa, sabuni za miche na karatasi za maliwato(toilet paper) majeruhi hao.
Akikabidhi
fedha hizo kwa niaba ya uongozi wa mkoa,Katibu tawala wake Eliya Ntandu alisema
mkoa umesikitiswa na kutokea kwa ajali hiyo huku akiendelea kusisitiza kuwa
mpango wa serikali ni kutokomeza kabisa ajali za vyombo vya moto kwa madereva
kuelimishwa juu ya usalama barabarani.
Kwa
upande wake Guninita alisema kuwa baada ya kupata taarifa ilibidi atoke Dar es
Salaam ili kuja kuwapa pole majeruhi ukizingatia kuwa yeye ni mzaliwa wa wilaya
hiyo hivyo kuguswa moja kwa moja na tukio hilo.
Guninita
aliwataka wananchi wengine kjitokeza kuwasaidia majeruhi walioendelea kulazwa
katika hospitali hiyo kwani wengi wao inaonekana wametoka nje ya Ifakara.
Awali
Afisa uhusiano wa hospitali ya Mt.Francis Nestoly Mlagani alisema mpaka sasa
chumba cha maiti umebaki mwili mmoja kati ya 11 ambapo 10 ilitambuliwa nadugu
kishwa kuruhusiwa kuendelea na taratibu za mazishi.
Ajali
hiyo ilitokea wiki iliyopita ilihusisha basi la kampuni ya Al Jabry lifanyalo
safari zake kati ya Morogoro na Ifakara kuligonga treni la Tazara maeneo ya
Kiberege na kusababisha vifo vya watu 12 huku wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa na
dereva wa basi hilo alifanikiwa kukimbia baada ya kusababisha ajali.
No comments:
Post a Comment