WAVUVI haramu
waliokuwa wakijaribu kuvua katika kisiwa cha Karange, kata ya Tangasisi, tarafa
ya Pongwe wilaya Tanga kwa kutumia baruti wamejeruhiwa na kukatika viungo vya miili
yao.
Tukio hilo limetokea Novemba 12, mwaka
huu majira ya saa 8:00 mchana.
Waliolipuliwa na kujeruhiwa na
baruti hiyo ni Hamisi Omari Kassimu (38) mkazi wa Mwambani ambae amekatika
mkono wa kulia na jicho la kulia, na Adamu Seleman Kapera (32) mkazi wa
Mwambani ambae amekatika mikono yote miwili, ameumia macho yote, vidole vinne
vya mguu wa kushoto na kuungua kifua.
Chombo kilichokuwa kinatumiwa kwenye
uvuvi huo haramu ni Ngalawa TTA 315. Hali ya majeruhi wote ambao wamelazwa kwenye
hospitali ya rufaa Bombo ni mbaya.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna mwandamizi msaidizi wa Polisi SACP Frasser Kashai alisema upelelezo unaendelea kuwabaini washirika wao na mtandao mzima wa wavuvi haramu kwa hatua za kisheria.
“Tunatoa wito kwa wananchi kutoa
taarifa kwenye vyombo vya usalama mara wanapowaona wavuvi wanaovua kinyume cha
sheria kwa kutumia baruti kitendo ambacho kinaleta madhara kwenye rasilimali
majini,” alisema Kashai na kuongeza
“Lakini pia samai hao wanaovuliwa
kwa baruti wanakwa na madhara makubwa
sana kwa afya za walaji, madhara ya baruti pia ni kama mnavyoona kwa
watu hao wanaotumia baruti hivyo basi taarifa zitolewe ili wahalifu
washughulikiwe.
No comments:
Post a Comment