MJUMBE
wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM MIZENGO PINDA ameitaka
Jumuiya ya Vijana ya Chama hicho UVCCM kuonyesha dhamira ya Kweli
katika kuimarisha mshikamano na umoja walionao.
Akifungua
semina ya siku tatu iliyowahusisha wajumbe wa baraza kuu la umoja huo Taifa
mjini Dodoma mheshimiwa PINDA ambaye pia ni waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania amesema umoja huo ndio ngome ya CCM hivyo wakishikamana
itakuwa rahisi kuwakatisha tamaa maadui.
Amesema
watu wengi wanapenda kuwaona wakifarakana lakini wasikubali na
wakatae jambo lolote lenye lengo la kudhoofisha umoja na mshikamano walionao
ili waweze kujipanga mapema kwa ajili ya ushindi.
Akizungumzia
kuhusu Katiba pendekezwa PINDA amesema vijana wanapaswa kutembea
vifua mbele na wasikubali kudanganywa kwa kuwa Katiba hiyo ni bora
na imeundwa kwa mfumo shirikishi.
Amesema
kazi iliyofanyika ni nzuri na wala hawataijutia ingawa kuna baadhi ya
wajumbe walitoka nje lakini kazi iliendelea na katiba pendekkezwa imepatikana.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa SADIFA JUMA HAMISI
amesema UVCCM ipo imara na wataenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
wakiwa wamoja na kuleta ushindi.
Mada
malimbali zinatarajiwa kuwasilishwa katika semina hiyo ikiwemo ushindi katika
uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na mada kuhusiana na katiba
Pendekezwa.
No comments:
Post a Comment