MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday, 25 November 2014

WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUGOMBEA UONGOZI




WANAWAKE wameshauriwa kutokuogopa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati akifungua baraza la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi UWT wilaya ya Mkinga.

Amewata kutokuogopa kujitokeza kuchukuwa fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye ngazi za vijiji,vitongoji na kata.

 Pia aliongeza kuwa ni wajibu wao kuhakikisha CCM inachukuwa nafasi zote za ugombea wa vijiji na kata kwenye wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine Naibu waziri aliweza kutoa kadi kwa wanachama 200 wapya waliotoka kwenye vyama vya upinzani.

No comments:

Post a Comment