JESHI la polisi mkoani Tanga linawashikilia watu watatu kwa kosa la kupatikana na Dola za kimarekani noti bandia 112 ambazo kama zingekuwa ni za halali zina thamani ya dola za kimarekani 11,200 ambazo ni sawa na milioni 20 kwa fedha za kitanzania .
Watuhumiwa hao Julius Kanza 30 mkazi wa Ubongo, Kenedy Binaga 35 mkazi wa Sinza, na Ramadhani Saddy 33 mkazi wa Mwenge walikamatwa wakiwa na gari yenye Chasis namba JLg 100037726
Akizungumza na wandishi wa habari kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Kamishna mwandamizi msaidizi SACP, Frasser Kashai kuhusiana na tukio hilo amesema limetokea Novemba 17 mwaka huu majira ya sa 7:30 mchana maeneo ya barabara ya 16 Kata na Tarafa ya Ngamiani Kati Wilayani Tanga.
No comments:
Post a Comment