MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Thursday, 4 December 2014

USHIRIKIANO WAZAZI NA WALIMU WA AWALI HUSAIDIA KUIBUA VIPAJI



USHIRIKIANO baina ya wazazi na walimu wa shule za awali ukiboreshwa unaweza kuibua vipaji na vipawa vya watoto wao.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha wanajombe waishio Jijini Tanga (UWANJOTA) Bernard Goliama kwenye sherehe za kuwaaga watoto wa shule awali ya Front Runner Day Care Centre iliyofanyika hivi karibuni kwenye hoteli ya Nyinda iliyopo eneo la Bombo mjijini hapo.

Goliama amesema kila mzazi na mlenzi nchini awajibike kuendeleza watoto kwa ngazi ya elimu ya awali  ili Tanzania iwe na wataalam wengi  waliyo na misingi imara ya masomo  yenye faida kwa manufaa ya  sasa na baadaye.

Hata hivyo hakusita kuwapongeza na kudhamini walimu na uongozi wa shule ya Front Runner Day Care Centre kwa jitihada ya kutoa elimu ya watoto hao ambao ni zaidi ya watoto 25 wamemaliza elimu hiyo ya awali kwa huu 2014.

Sambamba na hayo watoto wa shule hiyo kwa kupitia risala waliyosoma wamewaomba  wadau wa elimu kusaidiana na uongozi wa shule kuwajengea uzio wa shule hiyo ili waweze kusoma na kucheza kwa utulivu , furaha na amani.

No comments:

Post a Comment