MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Saturday 27 December 2014

KIVUKO MTO KILOMBERO CHAKUSANYA MIL. 776



KATIKA kipindi cha miezi 11 mwaka huu kivuko cha mto Kilombero kimeadaiwa kukusanya shilingi MIL 776,229,336 katika makusanyo yake wakati wa uvushaji watu na magari.

Hayo yalisemwa na mkuu wa kivuko cha mto Kilombero Mhandisi Fadhil HarounMeneja kwa niaba ya Meneja wa Temesa mkoa wa Morogoro Mhandisi Magreth Mapula kwenye kikao cha bodi ya kivuko hicho kinachotoa huduma ya kuvusha watu na vyombo vya usafiri viendavyo na kurudi wilayani Ulanga.

Katika ufafanuzi wake Haroun alisema mapato yamekuwa yakiongezeka na kushuka kutokana na msimu huku akifafanua kuwa mwezi Machi na Mei mapato yamekuwa yakishuka kutokana na hali ya mvua kusababisha barabara kutopitika kwa urahisi watu wengi kuwa mashambani kwa kilimo.

kwa mujibu wa meneja huyo kunachangamoto ya mafuriko na uharibifu mkubwa wa miundombinu,magari kugonga kivuko na kutumbukia majini,majani na nyavu kujisokota kwenye mfumo wa usukani wa kivuko na mchanga kujaa mtoni kunakosababisha kina kupungua.

Kwa upande wao wajumbe wa bodi ya kivuko hicho akiwemo mbunge wa jimbo la Ulanga magharibi Dk Haji Mponda walimtaka wakala wa ufundi na umeme Temesa mkoa wa Morogoro kuharakisha ujenzi wa vibanda vya kujikinga na mvua na jua kivukoni hapo.

Aidha walikitaka kivuuko hicho kuongeza pato lake ili kiweze kumudu kugharimia changamoto zinazojitokeza na kukifanya kuwa na tija katika utendaji wake.

Wazo hilo liliungwa mkono na mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala akionyesha masikitiko yake ya jinsi ambavyo mawazo ya bodi hayatekelezeki na kukatisha tamaa bodi hiyo kwa ushauri wake.

Aidha waliutaka uongozi wa usimamizi kivukoni hapo kutoa nafasi kwa vyombo vya usafiri vyenye abilia kupewa kipaumbele kupita kwanza kabla ya maroli ya mizigo hasa inapotokea kunakuwa na foleni.

No comments:

Post a Comment