MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Sunday 28 December 2014

MISS TANZANIA YAFUNGIWA KWA MIAKA MIWILI


SERIKALI ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.
 
Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.

Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.

Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.

Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.

Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

No comments:

Post a Comment