MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Wednesday 7 January 2015

WANNE WAUWAWA PONGWE KWA WIZI WA NG'OMBE



WATU wanne wameuawa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa Silaha za jadi baada ya kuwatuhumu kuiba Ng'ombe mmoja mwenye thamani ya shilingi laki saba.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Tanga Frasser Kashai amesema limetokea january 5 mwaka huu majira ya saa 20:00 usiku katika  kijiji cha Maranzara Tarafa ya Pongwe Wilayani Tanga.

Kamanda Kashai  amewataja watuhumiwa hao waliouawa kuwa ni Mwenshehe Abasi(29) na Edwin Kamugisha (25) wakazi wa  Pongwe Jamse Erick (22)mkazi wa Kange na Juma Bakari ambaye hajatambulika umri wala makazi .

imedaiwa kuwa baada ya ng'ombe huyo kuibiwa wananchi walifuatilia nyao zao na kuwakuta  watuhumiwa hao wanne wakimfunga ng'mbe huyo kwenye mti  ndipo wananchi hao walopoanza kuwashambulia hadi kuwauwa.

kufuatia mauaji hayo Jeshi  la Polisi limefanya Msako mkali na kufanikiwa kuwakamata  watuhumiwa watano wanaohusishwa na mauaji hayo ambao ni Abdi Mohamedi (29)  Kombo Mrami (23) Maendo Juma (20), Hakimu Omari (53) na Issa Bakari (53) na watuhumiwa wote watano ni wadigo wakazi wa Maranzara.

Miili ya marehemu watatu wamekabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya uchunguzi wa daktari na mwili mwingine bado umehifadhiwa katika hospital ya Mkoa Bombo ikisubiri utambuzi kutoka kwa ndugu watakao jitokeza.

No comments:

Post a Comment