BAADA ya kubainika sheria ndogo za
vijiji ‘by law’ kushindwa kuwawajibisha wanaokiuka taratibu wanasheria wa
halmashauri za wilaya wametakiwa kushirikiana na serikali kutengeneza na kuboresha
sheria zilizopo.
Hayo yamebainishwa na washiriki wa
mafunzo ya siku tatu ya ufuatiliaji na uwajibikaji wa jamii kwenye sekta ya
afya kwa washiriki 90 iliyojumuisha viongozi wa vijiji, kata, madiwani na
wananchi wa kawaida.
Semina hiyo iliyoanza juzi inaendeshwa
na shirika la Hale Development Organization HADEO.
Walisema hali hiyo imejitokeza baada
ya wanasheria wa halmashauri kutokuwa tayari kufika waliko wananchi hao na kushindwa
kushirikiana nao katika kutengeneza sheria zilizopo ama kuziboresha kwa manufaa
ya jamii.
Awali Diwani wa kata ya Magoma
Hadija Mshahara alisema iwapo watendaji watasimamia sheria kikamilifu hali ya
unyonge itaweza kuwaondokea.
Kauli hiyo ya diwani huyo ilichangiwa
na watendaji na wananchi wakielezea mapungufu ya kisheria yaliyopo hivi sasa
wakisema zimeshindwa kufanya kazi katika eneo la Mahakama ambapo mwezeshaji wa
semiha hiyo aliwakumbusha kwamba bado hilo liko kwenye uwezo wao na
halmashauri.
Katika semina hiyo ya mafunzo
iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu TTC wilayani Korogwe wafadhili wa
mafunzo hayo walikuwa ni shirika la The Foundation for civil society ambapo
shughuli ya mafunzo iliendeshwa na shirika la Hale Development Organization
HADEO la wilayani Korogwe.
No comments:
Post a Comment