MWANAMKE MAKINI BLOG

Advertise Here

Tuesday, 27 January 2015

MAGAIDI YA ALQAEDA WAWAPORA SMG POLISI


Na Mashaka Mhando,Tanga
MAJAMBAZI yanayohisiwa kuwa yamo kwenye mtandao wa Alqueda pamoja na kundi la Alshababu, imewajeruhi askari polisi na kuwapora bunduki mbili aina ya Sub-Machine Gun (SMG) zilizokuwa na risasi 60.

Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Juma Ndaki, limetokea katikati ya mitaa ya barabara ya 4 na 5 Jijini Tanga,  nyumbani kwa Jamali Twalib mwenye biashara ya kuuza chips Jijini hapa.

Polisi hao walioporwa bunduki hizo ni mwenye namba H 507 Konstebo Mwalimu na mwenzake G 369 Konstebo Mansur ambaye amelazwa katika hospitali ya Bombo baada ya kuchomwa kisu sehemu mgongoni na shingoni wakati wa uporaji huo na hali yake bado tete katika hospitali hiyo.

Mmoja ya mashuhuda wa tukio hilo, kijana muuza Chips Jeirus Chimya, alilieleza Majira kuwa tukio hilo lilitokea majira ya 5:45 usiku wakati askari hao waliokuwa na kawaida ya kula hapo wanapokuwa doria usiku, walifika wakaagiza chakula hicho.

"Kawaida askari hawa huwa wanafika wakiwa wanne na pikipiki zao na kula chakula hapa kila siku, sasa jana walifika wawili wakasema wenzao wamewaacha kituo cha basi cha Ratco watakuja wawawekee nao chakula chao, tukawaandalia kama kawaida," alisema Chimya.

Alisema baada ya kuwaandalia chakula kile ghafla waliwaona watu wanne wakiwafuata huku mmoja akiwa amebaki kwenye kona ya barabara ya 5 kutazama watu huku akiwa na pikipiki mbili ambazo walifika nazo kwenye tukuio hilo.

Chimya alisema askari wale walikuwa pembeni ng'ambo ya barabara kwenye duka moja linalouza nguo, wakikaa peke yao ndipo mmoja wa jambazi huyo alikuwa amevaa suruali wanayovaa askari wa Kutuliza ghasia FFU na kumvamia Mansur ambaye kwa wakati huo alikuwa akinywa soda.

"Yule jamba
zi aliyeonekana kama askari polisi alipoishika ile bunduki ya Mansur ambaye alitaharuki na jambazi kutoa kisu kwa lengo la kukata mkanda wa bunduki ili aondoke nayo akamchoma kisu cha shingo, lakini askari akawa mbishi akachomwa kisu kingine cha mgongoni akaiachia bunduki," alisema muuza chips huyo.

Aliendelea kueleza kwamba majambazi wengine wawili walimshika Mwalimu naye na kumpora bunduki yake na baada ya kuleta ubishi walimpiga na kisha kuangukia kwenye mtaro na kuichukua bunduki ile kirahisi na kukimbia katika eneo hilo.

"Kukweli watu tulioshuhudia tulipigwa na bumbuwazi tukizani ni utani baina ya askari kwa askari kutokana na namna walivyokuwa wamevalia watu wale kwani baada ya kupora bunduki hizo mmoja wa majambazi alishindwa kukimbia baada ya kupoteza funguo ya pikipiki.


Alisema baada ya muda askari wengine wawili waliokuwa wamewawekea chakula walifika katika eneo hilo huku majambazi wale wakiwa tayari wameondoka lakini wakafanikiwa kumkamata jambazi mmoja ambaye alikuwa akishindwa kuwasha pikpiki kutokana na kupoteza funguo.

Akizungumza ofisi kwake tukio hilo, kaimu kamanda wa polisi JUma Ndaki, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba mmoja wa majambazi waliomkamata na kumpekua nyumbani kwake walimkuta na CD zipatazo 13 zikiwa na mafunzo ya Alqueda na Alshababu.

"Ni kweli askari wetu wamenyany'anywa bunduki zikiwa na risasi 60 na mmoja wao tumemkamata na tulipompekua alikuwa na CD zenye kuonyesha mafunzo ya Alqueda bila shaka ni washirika wa kundi hilo na hivi sasa tunafanya mipango tumsafishe Jijini Dar es salaam kwa hatua zaidi za kiuchunguzi," alisema Ndaki.
Ndaki pia alisema walimkamata mmoja wa mke wa jambazi aliyemtaja kwa jina moja la Asha ambaye aliwahi kukamatwa kisha kuachiwa kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa Alqueda na kwamba kwa sasa mumewe ni mmoja kati ya waporaji wa bunduki hizo.

No comments:

Post a Comment