|
HALMASHAURI
ya mji wa Korogwe imefanikiwa kuwainua wanawake
na vijana kupitia mikopo ya fedha kupitia kwenye vikundi vyao.
Vikundi
hivyo vya wanawake na vijana vimepokea fedha hizo kwa kipindi cha mwaka
2014/2015 kwa ajili ya kupambana na umaskini na kuijiinua kiuchumi kupitia
mfuko wa maendeleo ya wanawake (WDF) na mfuko wa vijana (YDF).
Mkurugenzi
wa halmashauri wa mji wa Korogwe Lewis Kalinjuna wakati akisoma taarifa ya
mfuko wa wanawake na vijana mwaka 2014/2015 katika mkutano wa baraza la
madiwani uliofanyika mjini Korogwe amesema serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa
100% kwa kutumia fedha za makusanyo ya ndani.
“Hakuna
fedha yoyote iliyo pokelewa kutoka serikali kuu, halmashauri ya mji imejiwekea
utaratibu huu wa kuwapatia wanawake na vijana mikopo kupitia makusanyo yale ya
ndani kwa kila mwaka wa fedha,” alisisitiza Kalinjuna.
Amesema
fedha zilizotolewa na kukopeshwa kwa vikundi ni mili.60.3 ambapo kiasi
kilichokopeshwa kwa vikundi vya wanawake ni sh.mili.40.6 huku vikundi vya
vijana vikikopeshwa sh.mili.19.7 na sh.mili.19.7 ikiwa ni ya marejesho ya fedha
za mkopo hadi desemba 2014.
Jumla ya
vikundi vilivyokopeshwa ni 106, kati ya hivyo vikundi 72 ni vya wanawake na
vijana vikundi 34.
Mkurugenzi
huyo amesema katika halmashaurio hiyo mfuko huo umekuwa ukiwanufaisha wanawake
na vijana katika kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za ujasiriamali
ili kupunguza makali ya maisha na kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment