NA PAUL JAMES, TANGA
WATU wasiojulikana
wamevamia Ofisi ya Muhasibu katika shule ya St. Christina ya Jimbo katoliki la
Tanga iliyopo Kata ya Maweni, Tarafa ya Pongwe na kufanikiwa kuiba fedha
tasilim Mil 126 kisha kuichoma moto ofisi hiyo kwalengo lakupoteza ushahidi.
Tukio
hilo limetokea Januari 26, mwaka huu katika shule hiyo ambapo mwalimu wa shule
hiyo Mary Singano mkazi wa sahare aligundua uvunjifu huo na kutoa taarifa kwa
Jeshi la Polisi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Juma Ndaki alisema miongoni mwa fedha ziloibiwa ni
pamoja na karo za wanafunzi ambapo mpaka sasa jeshi la polisi lina mshikilia
mlinzi wa mahali hapo Jefta Mtiba na wanzanke watano ambao wanatiliwa mashaka.
Aidha
Ndaki amesema upelelezi unaendelea kuwabaini watu au mtu aliyehusika na uwizi
huo ili hatua zakisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Katika
hatua nyingine Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Kiwila Mbeya Hermany
Nyoni amefariki dunia papo hapo mara
baada ya kuligonga gari aina ya Volvo yenye namba za usajili T408CXB iliyokuwa
ikiendeshwa na Christopher John
mwenyeumri wa miaka (38) mkazi wa jijini Tanga
chanzo ikiwa ni mwendo kasi wa pikipiki.
Kaimu
kamanda Ndaki alisema tukio hilo la tarehe 27 Januari majira ya saa 3:30 usiku
limetokea katika eneo la Nguzo Tende Kwaminchi Kata ya Nguvumali Tarafa ya
Chumbageni barabara kuu ya Tanga-Muheza ambapo
marehemu alikuwa akiendesha pikipiki namba T115CQZ aliligonga gari hilo
lililokuwa maegesho kwa nyuma.
No comments:
Post a Comment